Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeElimuWanafunzi 29,193 kufanya Mtihani wa Upimaji wa Kidato cha Pili mkoani Shinyanga

Wanafunzi 29,193 kufanya Mtihani wa Upimaji wa Kidato cha Pili mkoani Shinyanga

Jumla ya wanafunzi 29,193 wanatarajiwa kufanya Mtihani wa Upimaji wa Kidato cha Pili mkoani Shinyanga, unaotarajiwa kuanza rasmi Novemba 10 hadi 19 mwaka huu katika shule mbalimbali za sekondari mkoani humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Afisa Elimu wa Mkoa wa Shinyanga, Samson Hango, kati ya wanafunzi hao, wavulana ni 12,103 na wasichana 17,090, huku watahiniwa 42 wakiwa ni wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Hango amewahimiza wazazi na walezi kuhakikisha wanafunzi wote waliojiandikisha wanahudhuria mitihani yao kwa wakati, akisema ni wajibu wa msingi wa kuhakikisha watoto wanatimiza malengo yao ya kielimu.

“Ni muhimu wazazi na walezi wakawapa wanafunzi motisha na kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kufanya mtihani huu kwa utulivu, kwani ni hatua muhimu katika maendeleo yao ya elimu,” alisema Hango.

Aidha, ametoa onho kali kwa walimu watakaobainika kujihusisha na vitendo vya udanganyifu au kuvuruga mchakato wa mtihani huo, akisisitiza kuwa mtihani huo ni wa kawaida wa kupima maendeleo ya wanafunzi kabla ya kuingia kidato cha tatu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments