Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ameialika Jumuiya ya Kimataifa kuwekeza katika sekta ya maji nchini Tanzania wakati akihutubia Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Maji na Maendeleo Endelevu unaofanyika jijini Dushanbe nchini Tajikistan.
Katika mkutano huo wa kimataifa wa “Water for Sustainable Development 2018–2028” ulioanza Mei 25 hadi 28, 2026, Waziri Aweso alimwakilisha Waziri Mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba.




Aweso amesema Tanzania inaendelea kukamilisha utoaji wa huduma ya maji katika vijiji 1,575 vilivyobaki kati ya vijiji 12,333 nchini, huku akisisitiza umuhimu wa kuimarisha uwezo wa taasisi, matumizi ya teknolojia pamoja na kutafuta vyanzo mbadala vya fedha kwa ajili ya sekta ya maji.
Aidha, amesema Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002 Toleo la 2025 pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 zimepanua ushiriki wa sekta binafsi katika maendeleo ya huduma za maji nchini.







