Friday, May 1, 2026
spot_img
HomeHabariDC Mtatifilo asisitiza utunzaji mazingira kuepuka magonjwa ya milipuko

DC Mtatifilo asisitiza utunzaji mazingira kuepuka magonjwa ya milipuko

Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Mtatifikolo, ameitaka Halmashauri ya Wilaya hiyo kuweka mikakati madhubuti ya utunzaji wa mazingira ili kusaidia kudhibiti na kuepuka magonjwa ya milipuko.

Akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, amesema kuwa utekelezaji wa mikakati hiyo utafanikiwa zaidi endapo utaanzia katika ngazi ya kata, ambako kuna idadi kubwa ya wananchi wanaoweza kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira.

Amebainisha kuwa usimamizi mzuri wa mazingira utasaidia kupunguza athari za kiafya pamoja na gharama zinazoweza kujitokeza kutokana na magonjwa ya mlipuko.

Aidha, amewataka madiwani kutoka halmashauri zote za Babati kuongeza juhudi katika kusimamia utunzaji wa mazingira katika maeneo yao, ili kulinda afya za wananchi na kuepusha athari za uharibifu wa mazingira.

Sambamba na hilo, Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza umuhimu wa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, ili kuhakikisha miradi ya maendeleo iliyobaki inakamilika kwa wakati na kuwanufaisha wananchi wa Wilaya ya Babati.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments