Saturday, November 8, 2025
spot_img
HomeHabariEWURA yatangaza bei mpya za mafuta nchini, yaonya wafanyabiashara watakaokiuka

EWURA yatangaza bei mpya za mafuta nchini, yaonya wafanyabiashara watakaokiuka


MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa Tanzania Bara zitakazotumika kuanzia leo, Novemba 5, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katika Bandari ya Dar es Salaam, petroli itauzwa kwa Sh 2,752 kwa lita, Tanga Sh 2,813, na Mtwara Sh 2,844 kwa bei ya rejareja.

Kwa upande wa dizeli, katika Bandari ya Dar es Salaam bei itakuwa Sh 2,704, Tanga Sh 2,766, na Mtwara Sh 2,797 kwa lita.

Katika baadhi ya mikoa ya ndani, Dodoma petroli itauzwa kwa Sh 2,831 na dizeli Sh 2,783 kwa lita, wakati Arusha petroli itauzwa Sh 2,861 na dizeli Sh 2,814 kwa lita.
Mkoani Mwanza, petroli itauzwa Sh 2,937 na dizeli Sh 2,890, huku Mbeya petroli ikipangwa kuuzwa Sh 2,884 na dizeli Sh 2,837 kwa lita.

EWURA imewakumbusha wafanyabiashara wote wa bidhaa za mafuta kuuza kwa bei zilizotangazwa, ikionya kuwa yeyote atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Pia, mamlaka hiyo imeagiza vituo vyote vya mafuta kuchapisha bei za bidhaa zao katika mabango yanayoonekana wazi, yakionesha bei halisi, punguzo au vivutio vya kibiashara vinavyotolewa, ili wateja waweze kuchagua vituo vinavyotoa huduma kwa bei nafuu zaidi na kuimarisha ushindani.

Aidha, EWURA imekumbusha kuwa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei ni kosa kisheria, na kituo chochote kitakachobainika kufanya hivyo kitapewa adhabu kali kwa mujibu wa kanuni.

Mamlaka hiyo pia imewataka wauzaji wa mafuta kutoa stakabadhi za mauzo kutoka kwenye Electronic Fiscal Pump Printers (EFPP), na wateja wahakikishe wanapokea stakabadhi hizo zenye taarifa kamili ikiwemo jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta na bei kwa lita.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments