HomeElimuHelios Towers yazindua maabara ya TEHAMA Shule ya Lupaso

Helios Towers yazindua maabara ya TEHAMA Shule ya Lupaso

MASASI, MTWARA — Kampuni ya Helios Towers imezindua rasmi maabara ya kisasa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika Shule ya Sekondari Lupaso, ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kurudisha kwa jamii kupitia uwekezaji katika elimu na maendeleo ya kidijitali nchini Tanzania.

Maabara hiyo iliyozinduliwa Mei 28, 2026, imefadhiliwa na Helios Towers Tanzania na kutekelezwa na Camara Education Tanzania kwa ushirikiano na uongozi wa shule pamoja na mamlaka za elimu za Wilaya ya Masasi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, uongozi wa mradi ulieleza kuwa maabara hiyo imegharimu zaidi ya Shilingi milioni 30 na imewekewa vifaa vya kisasa vya kujifunzia TEHAMA.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na kompyuta za mezani 25, projector, televisheni ya kidijitali (Smart TV), ubao mweupe (whiteboard), vifaa vya matengenezo ya TEHAMA (maintenance kit) pamoja na miundombinu ya mtandao wa ndani (LAN).

Kupitia mradi huo, zaidi ya wanafunzi 400 wa Shule ya Sekondari Lupaso wanatarajiwa kunufaika kwa kupata mazingira bora ya kujifunzia TEHAMA kwa vitendo, kuongeza uelewa wa teknolojia na kuimarisha ujuzi wa kidijitali utakaowaandaa kwa soko la ajira la sasa linalotegemea teknolojia.

Aidha, kama sehemu ya kuunga mkono utunzaji wa mazingira, Helios Towers imepanda miche 50 ya miti ya maembe na machungwa ndani ya shule hiyo, ikisisitiza kuwa elimu bora hupatikana katika mazingira safi na tulivu.

Uongozi wa kampuni hiyo umesisitiza kuwa uwekezaji huo ni sehemu ya dhamira yao ya kusaidia jamii katika maeneo ya elimu, teknolojia na maendeleo endelevu nchini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments