Mabinti wenye umri wa miaka 10 hadi 17 wanatarajiwa kunufaika na mafunzo maalum ya siku mbili yatakayofanyika jijini Dar es Salaam, yakilenga kuwajengea uwezo wa kujitambua, kujiamini na kukabiliana na changamoto za ukuaji katika mazingira ya sasa.
Mafunzo hayo yatakayofanyika Juni 9 na 10, 2026 katika eneo la Goba-Kibululu, yatajadili masuala muhimu ikiwemo kujitambua kijinsia, mabadiliko ya mwili, afya ya akili, elimu ya fedha, pamoja na matumizi salama ya simu, michezo ya mtandaoni na mitandao ya kijamii.

Waandaaji wa programu hiyo wamesema lengo ni kuwawezesha mabinti kuwa na maamuzi sahihi, kujitambua mapema na kujenga msingi imara wa mafanikio katika maisha yao ya baadaye.
Aidha, mafunzo hayo yatahusisha pia shughuli za kazi za mikono zinazolenga kukuza vipaji na kuwajengea mabinti ujuzi wa kujitegemea.




