Monday, May 4, 2026
spot_img
HomeHabariOthman aitaka ACT hekima kisiasa

Othman aitaka ACT hekima kisiasa

Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman, ameongoza kikao maalum cha Kamati Kuu kilichofanyika Magomeni jijini Dar es Salaam kujadili hali ya kisiasa nchini.

Akifungua kikao hicho cha dharura, amewataka viongozi wa chama kutumia hekima na weledi ili kuwasaidia Watanzania kufikia mafanikio, akidai wananchi wengi wamekata tamaa kutokana na mwenendo wa kisiasa wa sasa.

Amesisitiza kuwa viongozi wanapaswa kuacha lawama binafsi na badala yake kuangalia maslahi mapana ya taifa pamoja na matarajio ya wananchi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu, amesema kikao hicho ni cha dharura kikilenga kujadili mwelekeo wa kisiasa na kinatarajiwa kutoka na maazimio ya msimamo wa chama.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama, wakiwemo makamu wenyeviti Is-haka Mchinjita na Ismail Jussa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments