Tanzania inaendelea kuwa miongoni mwa nchi salama zaidi barani Afrika kwa ajili ya utalii, jambo lililochochea ongezeko kubwa la wageni wanaowasili kupitia Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA).
Kila wiki, mamia ya watalii kutoka mataifa mbalimbali duniani huwasili kupitia uwanja huo wakiwa na lengo la kutembelea vivutio vinavyopatikana Kanda ya Kaskazini ikiwemo Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Serengeti, Tarangire na Ziwa Manyara.
Wadau wa sekta ya utalii wanasema hali ya usalama, urafiki wa Watanzania, pamoja na sera thabiti za serikali katika kukuza utalii ni miongoni mwa sababu zinazowavutia wageni wengi.
Serikali imeendelea kuwekeza katika miundombinu ya anga na barabara ili kurahisisha safari za watalii kufika kwenye vivutio hivyo kwa urahisi.




