Treni ya Mwendokasi (SGR) imepata ajali asubuhi hii maeneo ya Ruvu baada ya kudaiwa kuhama njia wakati ikielekea mkoani Dodoma, ikitoka Dar es Salaam. Kwa mujibu wa abiria waliokuwemo kwenye treni hiyo wametoka salama licha ya kwamba wako baadhi waliopata majeraha madogo.
Msemaji wa Shirika la Reli (TRC) Fredy Mwanjala amekiri kupokea taarifa za ajali hiyo, na kwamba watatoa taarifa zaidi baadae baada ya kufanyika kwa tathmini ya kina.






