Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imesema Rais Samia Suluhu Hassan, alionesha dhamira ya kweli ya kufanya uchunguzi ili kupata ukweli.
Amesema Jumuiya ya Kimataifa inataka kufahamu mambo mawili ambayo ni kama Tanzania ina dhamira ya kufanya uchunguzi wa kina na uwajibikaji.
Mjumbe wa Tume hiyo, Prof. Ibrahim Juma, ameyasema hayo leo Aprili 28, 2026, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Kwa Rais Samia kuunda Tume ya Uchunguzi ni dhamira tosha kwamba tunataka kufanya uchunguzi, tunatafuta ukweli, tunatafuta ushahidi na tukishapata hizi taarifa ndio tunaamua suala la uwajibikaji,” amesema Prof. Juma.
Amesema hukumu ya Mahakama Kuu ilisema si kazi ya tume kutoa hukumu, kutaja waliohusika na akitajwa mtu akakimbilia Mahakama Kuu itaamuru aya zote zilizomtaja zifuwe.




