“Mfano; watoto wanaoishi katika mazingira magumu, waendesha pikipiki (bodaboda) na wajasiriamali wadogo walieleza kuwa walipewa fedha kati ya sh. 10,000 hadi sh. 50,000 na waliahidiwa ajira na maisha bora. Ilielezwa zaidi kuwa kuanzia tarehe 12 Oktoba, 2025 hadi 28 Oktoba, 2025 waliwekwa pamoja, kupewa mafunzo, kuandaliwa na kuhamasishwa kuwa sehemu ya kuanzisha na kushiriki ghasia siku ya Uchaguzi.”




