Katika kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za Msaada wa Kisheria kwa wakati na ysawa, Wizara ya Katiba na Sheria imeanza kutekeleza rasmi Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Awamu ya Pili.
Kampeni hiyo imeanza rasmi leo mkoani Dodoma kwa lengo la kutoa huduma za kisheria na elimu kwa wanachi wote hasa wale wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za huduma za Kisheria.


Katika awamu hiyo ya pili ya utekelezaji, Wizara ya Katiba na Sheria pamoja taasisi mbalimbali katika mnyororo wa haki jinai zinazoshiriki kutekeleza Kampeni hiyo, zitatoa huduma mbalimbali ikiwamo ushauri wa kisheria, utatuzi wa migogoro ikiwamo ya ardhi, ndoa,mirathi, matunzo ya watoto na masuala ya ukatili wa kijinsia.
Kampeni hiyo inayoendeshwa bila malipo ya Msaada wa Kisheria, katika mkoa wa Dodoma, inatekelezwa kwa siku 15 katika Halmashauri zote nane za mkoa huo ikijumuisha Kata,Mitaa na Vijiji vyote vya mkoa huo.





