Saturday, April 25, 2026
spot_img
HomeHabari‎ Dk. Samia: Tumedhamiria kukuza uvuvi, kuzalisha ajira

‎ Dk. Samia: Tumedhamiria kukuza uvuvi, kuzalisha ajira

Rais Dk Samia Suluhu Hassan, amesema amedhamiri kulifufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), ili liwe na uwezo wa kusimamia uvunaji wa rasilimali za bahari kuu.

Mkuu huyo wa nchi, ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo, Jumamosi Aprili 25, 2026 alipozungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa meli ya kwanza ya uvuvi wa bahari kuu.

‎“Tumedhamiria kulifufua na kuliimarisha Shirika letu la uvuvi TAFICO, ili liweze kushiriki ipasavyo kusimamia uvunaji wa rasilimali za bahari kuu,” amesema.

‎Kwa muda mrefu, amesema uvunaji wa rasilimali za bahari kuu umekuwa ukifanywa na meli na kampuni kutoka nje na kuzorotesha uwezo wa nchi kunufaika na mapato ya rasilimali zake.

‎Amesema kuliwezesha shirika hilo kwa vifaa na teknolojia za kisasa ni muhimu na jambo la lazima na Serikali inafanya hivyo ili kuiwezesha nchi na wananchi kunufaika na fursa zitokanazo na rasilimali za uvuvi wa bahari kuu..

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments