HomeBiasharaURUS Tanzania yawafikia wafugaji na wahimilishaji zaidi ya 20,000

URUS Tanzania yawafikia wafugaji na wahimilishaji zaidi ya 20,000

Ikiwa ni sehemu ya kusaidia jitihada za kukuza sekta ya mifugo hapa nchini, kampuni ya URUS Tanzania, imefanikiwa kuwafikia wafugaji na wahimilishaji zaidi ya 20,000 Tanzania bara na visiwani.

URUS Tanzania, ni kampuni tanzu ya URUS global yenye makao makuu yake nchini Marekani. Pamoja na shughuli nyingine, kampuni hii inayojihusisha na usambazaji wa mbegu bora za ng’ombe wa maziwa na nyama katika nchi mbvali mbali duniani ikiwamo Tanzania.

Akiongea kwenye maonesho ya mifugo yanayofanyika Ubena Zomozi Chalinze mkoani Pwani, meneja mkazi wa URUS Tanzania Edson Mfuru alisema lengo la kuyafikia makundi hayo ni kusaidia upatikanaji wa elimu na teknalojia za kisasa zinazoweza kuongeza tija kwenye sekta ya mifugo.

‘Lengo letu ni kusaidia kuongeza uzalishaji wa bidhaa za mifugo kama nyama na maziwa kupitia teknalojia rahisi,rafiki na yenye ufanisi ya uhimilishaji. Teknalojia tunayoitumia inawezesha kupatikana kwa ng’ombe chotara wa nyama na maziwa wenye uwezo wa kuzalisha maziwa zaidi pamoja na nyama kuliko ng’ombe wetu wa kienyeji,” alieleza

Meneja huyo aliesema teknalojia hiyo tayari imeshaanza kutumika hapa nchini na kuongeza kuwa baadhi ya wafugaji wamenufaika nayo huku jitihada zaidi zikifanyika kuwafikia wafugaji katika sehemu nyingi zaidi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments