Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali imeanza kulipa malimbikizo ya madeni ya hifadhi ya jamii, posho za likizo na uhamisho.
Pia, imeanza kulipa na itaendelea kulipa malimbikizo ya mishahara, akiahidi mchakato kuwa endelevu kulingana na tathimini inayoendelea.
Dkt Samia ameeleza hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi’, yaliyofanyika kitaifa mkoani Njombe.
“Hatuletewi madai tukalipa hapo hapo, lazima tutathimini na yale yanayothibitika ni halali tumeanza kuyalipa,” amesema Rais Dkt Samia.




