Rais Samia Suluhu Hassan, alivyowasili mkoani Iringa kwa ajili ya kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi yanayotarajiwa kufanyika mkoani Njombe leo Mei 1, 2026.
Rais Samia amepokelewa na viongozi wa serikali wa mkoa pamoja na wananchi, kabla ya kuelekea Njombe ambako maadhimisho ya kitaifa ya Mei Mosi yanafanyika mwaka huu.
Maadhimisho hayo hukutanisha wafanyakazi, waajiri na serikali kujadili masuala ya ajira, maslahi ya wafanyakazi na mchango wao katika uchumi wa taifa.






