Friday, December 5, 2025
spot_img
HomeHabariNaibu Waziri, Salome Makamba atua EWURA, atoa maagizo

Naibu Waziri, Salome Makamba atua EWURA, atoa maagizo

Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, leo amekutana na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuteuliwa katika nafasi hiyo hivi karibuni.

Makamba amekutana na viongozi hao kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali ya utendaji na maboresho ya sekta ya nishati nchini katika Ofisi za Makao Makuu ya EWURA jijini Dodoma.

Aidha, ameipongeza EWURA kwa kazi nzuri katika kusimamia huduma za nishati, na kuitaka Mamlaka hiyo kuongeza kasi, ubunifu na ufanisi.

“Mimi si muumini wa kushindwa, hivyo natoa rai kwenu kujipanga ili kuendana na kasi hiyo, ili muendelee kung’ara katika uendeshaji wa shughuli zenu” amesema.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk. James Andilile, amewasilisha mbele ya Makamba taarifa fupi kuhusu majukumu ya Mamlaka, mafanikio yaliyopatikana, pamoja na maeneo yanayoendelea kuimarishwa.

Dk. Andilile ameahidi taasisi yake kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, salama na za uhakika.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments