Sunday, January 25, 2026
spot_img
HomeHabariSamia: Hakuna aibu CCM kusafirisha wanachama kwenda mikutano ya kampeni

Samia: Hakuna aibu CCM kusafirisha wanachama kwenda mikutano ya kampeni

Mgombea wa urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, amesema hakuna tatizo wala aibu kwa chama hicho kusafirisha wanachama wake kwa magari ili kuhudhuria mikutano ya kampeni.

Akihutubia leo, Septemba 5, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Tukuyu, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Samia alisema hatua hiyo inalenga kusaidia wanachama wanaoishi maeneo ya mbali kufika kwa urahisi kwenye viwanja vya mikutano.

“Ni Wajibu Wetu Kuwasaidia”

“Nimesikia waandishi wa habari jana (juzi) wakimwambia Mwenezi kwamba CCM kinasafirisha watu kwa magari ndio maana mikutano inajaa. Lazima tutoe watu. Huwezi kutegemea mtu atoke umbali wa kilometa 90 au 100 kwa miguu hadi kufika hapa Uwanja wa Tandale. Ni lazima tuwasaidie usafiri. Lakini hatutoi watu kutoka wilaya moja kwenda nyingine, tunasafirisha waliomo ndani ya wilaya husika,” alisema Samia.

Aliongeza kuwa hatua hiyo si kosa bali ni msaada wa kimsingi kwa wananchi wenye hamu ya kusikiliza sera na utekelezaji wa ilani ya chama hicho.

“Siyo Shida Wala Aibu”

Samia alisisitiza kuwa hakuna sababu ya kuiona hatua hiyo kama udhaifu au hila ya kujaza mikutano, bali ni jitihada za kuwezesha ushiriki wa wananchi.

“Siyo shida wala siyo aibu kwa chama kusafirisha wanachama wake kuja kusikiliza ilani ya chama inasemaje na yale tuliyoyatekeleza,” aliongeza.

Shukrani kwa Wananchi

Akihitimisha hotuba yake, Samia aliwashukuru wakazi wa Tukuyu na Rungwe kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mkutano huo wa kampeni, akisema idadi kubwa ya wananchi waliokuja ni uthibitisho wa imani waliyonayo kwa CCM.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments