Tuesday, April 28, 2026
spot_img
HomeHabariWatano wakamatwa kwa utapeli Tabora

Watano wakamatwa kwa utapeli Tabora

Jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, linawashikilia watu watano kwa tuhuma za wizi wa Sh milioni 40.

Inadaiwa kuwa, watuhumiwa hao walijipatia fedha hizo baada ya kumlaghai na kumtapeli mfanyanyabiashara, Fatuma Nasoro mkazi wa Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.

Watu hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti wakiwa ndini ya mkoa wa Tabora wakiendelaa na majukumu yao ya kawaida.

Akielezea tukio hilo leo Aprili 28, 2026 katika mkutano wake na waandishi wa habari, Mkuu wa mkoa wa Tabora, Paul Chacha amesema wamefanikiwa kuwakamata watu hao watano ambao kati yao wawili waliofahamika kwa majina ya Marseli Gwasima na Fred Ricardo waliojifanya wahudumu wa kampuni ya mawasiliano nchini (jina linahifadhiwa) walimtapeli mfanyabiasahara huyo fedha hizo.

“Fatuma ambaye ni mfanyabiashara wa khanga na kitenge wilayani Kaliua alitapeliwa na watu hao majuma kadhaa yaliyopita kwa kuhamisha fedha hizo kutoka kwenye akaunti ya Banki na kupeleka kwenye namba zao za simu,” amesema Chacha.

“Kimsingi vijana hawa walijitambulisha kama wahudumu wanaotembea mitaani kwa ajili ya kusajilia wafanyabiashara Lipa Namba, niendelee kutoa onyo kwa matapeli na wahalifu wote kwamba binafsi sitapepesa macho matukio yoyote yale ya kihalifu katika mkoa wa Tabora,” ameongeza.

Amesema kuwa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Tabora ipo macho muda wote na itaendelea kulinda raia wote wa Tabora pamoja na mali zao.

RC Chacha ametoa rai kwa wakazi wote wa mkoa huo kuwa waangalifu pale ambapo wanatafuta huduma za aina hiyo kutoka kwa watu wanaojitambulisha kama mawakala au wahudumu wa kampuni za mawasiliano.

Kwa upande wake, mhanga wa tukio hilo, Fatuma Nasoro ameishukuru kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Tabora kwa kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao, huku akiomba huta kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao na iwe fundisho kwa watu wengine wenye vitendo viovu kama hivyo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments