Thursday, April 23, 2026
spot_img
HomeHabariTume: Wafanyavurugu walikuwa na vilipuzi, bunduki

Tume: Wafanyavurugu walikuwa na vilipuzi, bunduki

Tume ya uchunguzi wa ghasia wakati na baada ya uchaguzi, imesema walioshiriki vurugu za Oktoba 29, 2025 walikuwa na silaha mbalimbali ikiwemo bunduki na vilipuzi.

Hayo yameelezwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi Aprili 23, 2026 na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Othman Chande, alipozungumza wakati wa kuwasilisha ripoti ya uchunguzi kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

“Washiriki wa ghasia za wakati na baada ya uchaguzi mkuu walibeba silaha za aina mbalimbali zikiwemo mawe, nondo, mkuki, sururu, fimbo, marungu, visu, viberiti, vilipuzi, bunduki, manati, kombeo, rato na mapanga jambo ambalo haliruhusiwi kisheria katika maandamano ya amani,” amesema.

Amesema kitendo hicho ni kinyume na Ibara ya 21 ya Mkataba wa Haki za Kiraia na Kisiasa, 1966, na sheria nyingine za kitaifa na kikanda, kadhalika Katiba ya Tanzania.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments