Mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dkt. Fredrick Shoo amesema ameipokea ripoti ya Tume ya Uchunguzi kwa furaha kwani imeliponya Taifa kutoka kwenye majeraha yaliyotokea Oktoba 29, 2025 kwa kuongea ukweli na kutoa mapendekezo ambayo Serikali ikiyafanyia kazi basi Tanzania itazidi kuwa kisiwa cha Amani.




