Sunday, April 26, 2026
spot_img
HomeHabariMSD kuingiza dawa ya kuacha pombe

MSD kuingiza dawa ya kuacha pombe

Bohari ya Dawa MSD imetangaza mpango wa kuingiza nchini dawa maalum ya kusaidia watu wenye changamoto ya uraibu wa pombe.

Akizungumza Aprili 24, 2026 jijini Dodoma, Meneja wa MSD Kanda ya Dodoma, Mwanashehe Jumaa, amesema dawa hiyo italetwa kwa kushirikiana na Hospitali ya Mirembe.

Amesema hapo awali dawa hizo zilipatikana kwa shida katika baadhi ya famasi, lakini sasa zitapatikana kwa urahisi zaidi kupitia MSD kwa gharama nafuu ili kuwasaidia wagonjwa wengi.

“Tumeipata dawa hii kwa gharama nafuu, na itasambazwa ili kurahisisha upatikanaji wake kwa wahitaji,” amesema.

Amebainisha kuwa dawa hiyo inalenga kusaidia kuacha uraibu wa pombe pekee na si sigara, huku akieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za kuboresha huduma za afya ya akili na uraibu nchini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments